Mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam amewaonya wanaume waliokataa wito wa kuitwa kwao kuhusiana na malezi ya
mtoto kufanya hivyo mara moja, la sivyo anapeleka majina yao kwa Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam Lazaro Mambosasa, ili wakamatwe na kuchukuliwa
hatua za kisheria.
Makonda ametoa kauli hiyo alipokuwa
akiongea na kina mama ambao wametelekezwa kulea watoto na baba wa watoto
waliozaa nao, na kusema kwamba muda wa kubembelezana umkwisha, kinachofuata ni
kuhakikisha wanaume hao wanakamatwa na jeshi la polisi ili kuwawajibisha.
“Kwa mwanaume yeyote ambaye
amepigiwa simu, amepelekewa barua halafu amakaidi wito, kuanzia Jumatatu
ninawakamata wanaume waliokimbia majukumu yao, ambao hawajafika, siku ya
Jumapili majina yao wote yataenda kwa Mambosasa, na mtaanza kushughulikiwa,
siwezi kuongoza mkoa unaendelea kuwa na idadi ya watoto ombaomba wakati baba
zao wapo”, amesema Paul Makonda.
Pia Paul Makonda amesema hafanyi
hivyo kwa ajili ya kuwatetea wasaidizi wa kazi (house girl) aliyelala na baba
mwenye nyumba au katibu muhtasi (secretary) aliyetembea na bosi, bali anafanya
hivyo kwa ajili ya kuwasaidia na kuwalinda watoto ambao hawana hatia.
“Na simtetei housegirl aliyelala na
baba mwenye nyumba akavunja ndoa, simtetei secretary aliyelala na bosi wake
akafanya mpaka akapanda cheo, ninayemtetea ni mtoto aliyezaliwa bila kuchagua
kuzaliwa hapo”, amesema Paul Makonda.
Waliokataa wito wa Makonda Kupelekwa mikononi mwa kamanda Mambosasa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment