Ummy awashukuru wabunge kwa bilioni 898


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Mh. Ummy Mwalimu amewashukuru Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupitisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2018/19.

''Nawashukuru Wabunge kwa kupitisha Bajeti ya Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2018/19'', amesema Mh. Ummy siku moja baada ya bunge la bajeti kwa pamoja kupitisha bajeti hiyo. 

Mbali na shukrani hizo Mh. Ummy pia ameahidi kufanyia kazi ushauri ambao umetolewa na wabunge hususani kwenye uboreshaji wa huduma za afya pamoja na miundombinu yake nchini kote.

''Tutafanyia kazi maoni na ushauri wenu ili kuboresha huduma za Afya na Ustawi wa jamii nchini hasa kwa wananchi wa kipato cha chini katika maeneo ya vijijini ili waweze kunufaika na bajeti hii'', ameongeza.

Vipaumbele vya bajeti ya wizara hiyo ambayo imetengewa jumla ya shilingi bilioni 898 ni Chanjo, Kinga, Magonjwa yasiyoambukiza, Afya ya uzazi, Damu salama, Dawa na vifaa tiba, Hospitali za Mikoa na Kanda pamoja na Vituo vya Afya.

Ummy awashukuru wabunge kwa bilioni 898 Ummy awashukuru wabunge kwa bilioni 898 Reviewed by KUSAGANEWS on April 21, 2018 Rating: 5

No comments: