KUNDI LA FRIENDS OF BATULI TUENDELEE KUIGUSA JAMII INAYOISHI MAZINGIRA MAGUMU KWA KADRI WANAVYOBARIKIWA
Msemaji wa kundi la Friends of batuli akikabidhi uniform
za wanafunzi kwa mmoja wa walimu ambazo zimetolewa na kundi hilo katika shule ya Msingi ungalimitedi
jijini Arusha Picha Na Alphonce Kusaga
Mmoja wa wanafunzi anayeishi mazingira magumu akifurahia msaada alioupata kutoka
kundi la Friends of batuli katika shule ya msingi Salei kata Ungalimitedi jiji la
Arusha
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Salei Niminini kahema akipokea msaada kutoka kwa wadau wa kundi la Friens Of Batuli kwa ajili ya kukabidhi watoto wa shule hiyo wenye mazingira magumu
Katibu wa kundi la friends of Batuli Tausi Swalehe pamoja na msemaji
wake Batuli Kisaya na mmoja wa mdau wa kundi hilo wakikabidhi msaada shule ya msingi
Ungalimitedi.
|
Jamii imetakiwa kuthamini na kuwa karibu na makundi
maalum kwa kuonyesha upendo ,faraja pamoja na ushirikiano ili makundi hayo
wajisikie kama watu wengine ambao hawana matatizo.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa kundi la Friends Of Batuli
Bi Batuli Kisaya wakati wakikabidhi misaada ya Nguo za Shule,Chakula pamoja na
vifaa vya Shule katika shule za msingi Ungalimitedi na Salei zilizopo katika
kata ya Ungalimitedi katika halmashauri ya jiji la Arusha ambapo amesisitiza
kuwa jamii ina nafasi ya kubadilisha maisha ya makundi maalum.
Batuli amesema kuwa kundi hilo limekuwa wahamasishaji
wakubwa katika kufikia makundi maalum licha ya kuwa hawana vitu vikubwa vya
kutoa lakini wanatoa kadri ya walivyobarikiwa na mwenyezi Mungu.
Amesema kuwa wametoa vitu mbalimbali kama vile Mafuta ya
kupikia ,mchele,Nguo za shule,madaftari ,Soksi ,masweta ya Shule,sukari ,sabuni
na vitu vingine jumla vina thamani ya shilingi Milioni moja.
Batuli ameongeza kuwa amesema kuwa hakuna jambo
linaloshindikana endapo jamii itaamua kusaidia makundi maalum ambapo mpaka sasa
wameshatoa msaada kwenye vituo vyenye makundi maalum zaidi ya 35 licha ya kuwa
hawana chanzo cha mapato.
Hata hivyo makamu mwenyekiti wa kundi hilo la Friends of
Batuli Bwana Aly bwanga amesema jamii inatakiwa kuwa mstari wa mbele kutambua
jamii yenye uhitaji maalum kwasababu hazikupenda kuishi hivyo ambavyo wanaishi
kwasasa.
Bwanga amesisitiza kuwa kila mtu anapokaa katika maeneo
yanayomzunguka kuna watu wanahitaji msaada kupitia yeye kwa kuguswa kutoa kitu
hata kikiwa kidogo.
Akizungumza baada ya Kupata misaada hiyo mwalimu mkuu wa
shule ya Ungalimitedi Emanuel Kileo amesema katika shule hiyo kuna watoto zaidi
ya 400 ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ambao wanahitaji
msaada kutoka kwa wadau ikiwemo kundi la Friends Of Batuli.
Naye mwalimu mkuu wa shule ya msingi Salei Niminini
kahema ameshukuru kundi hilo la Friends of batuli huku akiitaka jamii kutoa
msaada kila wakati bila kusubiri kipindi maalum kama kwenye sikuu za mfungo wa
ramadhani ,sherehe za kidini pamoja na sherehe malum.
“Mimi nafikiri tusitegemee siku za Special Days iwe
mwaka mzima kwamba hizi kazi zifanyike mwaka mzima kwasababu mahitaji ya watoto
hayategemei siku za siku kuu tu mwaka mzima hawa watoto wana shida tunajitoa
hata sisi kama walimu kuna wengine hawana viatu hawana nguo za shule ,viatu
yani hawana kabisa kitu hiki kitendeke mwaka mzima unapobarikiwa toa tusisubiri
hizo siku kuu mara nyingi wengi wanasubiria Idi ,na Krismas Jamani shida hazina
Krismas tuna jambo la kuiga kutoa kwenu friends of batuli”Mw/mkuu shule ya
Salei Niminini Kahema
Kwa upande wa Shekhe wa wilaya ya Arusha Dc Shekh
Hussein Saidi Ijunje amesema kuwa wanachokifanya kundi la Friends of Batuli ni
jambo ambalo linatakiwa kuigwa na kila mmoja katika jamii kwa kuwa hata
maandiko matakatifu yamelekeza kusaidia makundi maalum.
Shekh Hussein amesema makundi mbalimbali ambayo yapo
yaige mfano wa kundi hilo kwa kuhakikisha wanatenga kitu kidogo kwa ajili ya
kusaidia makundi yenye mahitaji maalum.
Licha ya kutembelea shule Mbili za msingi Ungalimitedi
pamoja na shule Salei pia wametembelea kituo cha CHISEA kilichopo kata ya
ungalimitedi jijini Arusha ambapo kituo hicho wameshukuru kwa msaada wa kutoka
kwa kundi hilo
KUNDI LA FRIENDS OF BATULI TUENDELEE KUIGUSA JAMII INAYOISHI MAZINGIRA MAGUMU KWA KADRI WANAVYOBARIKIWA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment