DC atishia kufungia viwanda

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva amesema yuko tayari kukifungia kiwanda chochote katika wilaya hiyo kitakachoonekana kuendesha shughuli zake bila kuzingatia haki za wafanyakazi

Lyaviva ameyasema hayo leo Aprili 21, 2018 alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Chemba ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) wa Mwaka 2018

Lyaviva amesema katika kipindi cha uongozi wake, tayari amepokea kesi 246 za migogoro ya wafanyakazi katika viwanda vilivyopo wilayani hapo

Kwa mujibu wa DC Lyaviva, idadi ya viwanda katika wilaya hiyo ni wastani wa 400, kuanzia vikubwa, vya kati na vidogo vidogo

"Katika kesi hizo kuna wafanyakazi wanalalamikia kunyimwa mikataba, kutolipwa mishahara yao kwa wakati, kuna kingine nimebaini ukienda kuomba kazi unaombwa vyeti vyako lakini siku ukitaka kuondoka inakuwa shida kupewa," amesema

Ameongeza: "Kwa hiyo hatuwezi kukaa na kiwanda kinachokandamiza wafanyakazi, hukujali sheria za nchi, lakini tatizo kubwa ni HR (maofisa wa rasilimali watu), wanalinda maslahi ya waajiri wao tu badala ya kuwa kiunganishi kati wafanyakazi na waajiri. Naagiza HR waanze kushughulikia kero hizo."
DC huyo ametumia muda mwingi kuwataka kujenga utamaduni wa kulipa kodi kwa Maendeleo ya Taifa
TCCIA-Temeke yenye wanachama wastani wa 500, imewakutanisha wanachama katika mkutano huo kwa lengo la kujadili mafanikio, changamoto katika utendaji kwa mwaka 2017 na kuweka mikakati mipya kwa mwaka 2018 ili kufikia malengo

Wadau wengine walioshiriki mkutano huo wa siku moja ni Mamlaka ya Chakula na Dawa,(TFDA) Mamlaka ya Mapato (TRA) Benki ya NMB na Wakala wa Usajili wa Kampuni (Brela) ambao watatoa msaada mbalimbali ili kupata mwongozo wa mabadiliko ya kisheria katika shughuli za kibiashara.
DC atishia kufungia viwanda DC atishia kufungia viwanda Reviewed by KUSAGANEWS on April 21, 2018 Rating: 5

No comments: