Wakati chanjo ya saratani ya
mlango wa kizazi kwa wasichana wote wenye umri wa miaka 14 ikitarajiwa kuanza
kutolewa Jumatatu wiki ijayo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
amesema ana mikakati ya kupita nyumba kwa nyumba ili kuwapima wanaume
saratani tezi ya dume
Makonda ameyasema hayo leo Aprili
21 wakati akifungua rasmi warsha ya chanjo hiyo iliyowashirikisha waandishi
wa habari, wataalamu wa afya, viongozi mbalimbali wa dini na siasa
Amesema wakati saratani ya mlango
wa kizazi ikiwaathiri wanawake nchini, tezi dume inaumiza zaidi akina baba
ambao hata hivyo hakuna mwamko wa kulizungumzia jambo hilo katika
jamii.
"Kuna kasumba kuwa saratani
ya tezi dume inapimwa kwa kidole jamani siyo kweli, kuna kipimo cha damu na
ni rahisi hivyo nina mkakati wa kupita nyumba kwa nyumba katika mkoa wangu
kuhakikisha hii kasi ya vifo kwa kinababa inapungua kwa kuwagundua mapema na
kuwaanzishia matibabu," amesema Makonda.
Pia, ametoa wito kwa viongozi wote
wa serikali za mitaa na viongozi wa dini kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii
ili wasichana wote wenye umri huo wafike kwenye vituo kwa wingi kupata chanjo
Makonda amesisitiza pia kuzingatia
kupata chanjo kamili kwa kurudi mara ya pili ili kuikamilisha.
|
|
Makonda kupima tezi dume nyumba kwa nyumba
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment