Dada wa Masogange asema atakapozikwa Masogange

Siku moja baada ya msanii anayepamba video za muziki wa Bongo Fleva nchini, Agness Gerald, maarufu Masogange, kufariki dunia dada yake amesema wataifuata ratiba ya msiba kama ilvyopangwa na wasanii wenzake

Akizungumza leo Aprili 21 dada wa marehemu, Flora Gerald amesema, wataifuata ratiba ya msiba huo kwa hapa Dar es Salaam, kama wasanii wenzake walivyosema

“Kama wenzake walivyosema, ataagwa viwanja vya Leaders kesho na baada ya hapo atasafirishwa kwenda Mbeya na Jumatatu atazikwa nyumbani kwa baba yake,” amesema

Hata hivyo Flora hakuweza kuzungumza kwa kina kutokana na kujawa na majonzi

Mpaka saa nane mchana leo, wasanii waliojitokeza wenye majina makubwa walikuwa ni Dogo Janja na Irine Uwoya ambaye anaishi nyumba aliyokuwa anaishi Masogange

Jana Steve Nyerere alizungumza amesema kuwa Masogange ataagwa kesho na kusafirishwa kwenda Mbeya kwa maziko.
Dada wa Masogange asema atakapozikwa Masogange Dada wa Masogange asema atakapozikwa Masogange Reviewed by KUSAGANEWS on April 21, 2018 Rating: 5

No comments: