WAFUASI 24 WA CHADEMA WARIPOTI POLISI


Wafuasi 24 wa chadema waliokamatwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam  Jumanne iliyopita wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi leo Jumatano Aprili 11, 2018 

Akizungumza nje ya kituo hicho, Ofisa wa Kanda ya Pwani Chadema, Jerry Karege amesema waliitikia wito wa polisi na walipofika 
walielezwa kuripoti kwa  mkuu wa upelelezi wa polisi mkoa wa Ilala

Karege amesema walipofika kwa mkuu huyo wa upelelezi walitakiwa kuripoti tena kituoni hapo  Aprili 13 mwaka huu

"Sisi tumeitikia wito wa polisi lakini hatujaambiwa kitu chochote zaidi ya kutakiwa kuondoka na kuripoti tena siku ya Ijumaa,” amesema Karege.

WAFUASI 24 WA CHADEMA WARIPOTI POLISI WAFUASI 24 WA CHADEMA WARIPOTI POLISI Reviewed by KUSAGANEWS on April 11, 2018 Rating: 5

No comments: