Idara ya uhamiaji mkoani
Dodoma inawashikilia raia tisa wa kigeni kutoka mataifa mbalimbali wakiwemo
wachezaji wanne wa mpira wa miguu kutoka Nigeria ambao waliingia nchini kwa
lengo la kufanya majaribio na timu mbalimbali ili wasajiliwe.
Afisa uhamiaji katika mkoa huo Peter
Kundy amesema raia wanne wa Nigeria waliingia nchini na wakala Gabriel Nkayimbo
raia wa Cameroon ili wasajiliwe na klabu ya African Lyon ya jijini Dar es
Salaam au Dodoma FC ya Dodoma lakini baada ya kushindwa wakatelekezwa.
Kundy amesema raia hao wametakiwa
kuondoka nchini mara moja ambapo raia wengine wanaotoka mataifa ya Burundi,
Uganda na Sudan kusini nao wametakiwa kuondoka nchini na kutoa rai kwa mawakala
wa wachezaji kufuata utaratibu uliopo wa TFF na FIFA pamoja na wamiliki wa
shule, saluni na nyumba za kulala wageni kutowapokea wageni wasiofuata taratibu
za nchi.
Mbali na hilo, Jeshi la Polisi mkoa
wa Dodoma limewakamata watuhumiwa 23 wa makosa mbalimbali yakiwemo ya wizi wa
kuvunja nyumba, uvutaji bangi, mirungi na utapeli baada ya kufanyika msako
ndani ya mji huo.
Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma,
Gilles Muroto akizungumza na waandishi wa habari amesema watuhumiwa hao
wamekamatwa wakiwa na mihuri ya mabenki mbalimbali, vitambulisho, nywele za
akinamama, bangi, luninga na mirungi.
Wachezaji wanne washikiliwa na Uhamiaji Dodoma
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 05, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment