Mufti wa Tanzania Sheikh
Abubakari Zuberi amesema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limefanya
mabadiliko ya upatikanaji wa viongozi kwa nchi nzima kuanzia ngazi ya Masheikh
wa wilaya, mikoa na Taifa.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam
wakati akitoa maazimio ya kikao cha Baraza Kuu la BAKWATA kikao kilichokaa
Mjini Dodoma mwishoni mwa mwezi Machi, Mufti amesema wamekubaliana kwa kauli
moja kuwa upatikanaji wa viongozi wa Kiislamu utakua ni wakuteuliwa na sio
kuchaguliwa tena kama ilivyo sasa.
Amesema Mkutano Mkuu uliofanyika
tarehe Machi 31 - Aprili 1 umesema kuwa mfumo wa uchaguzi hauwaachi watu salama
sana sana husababisha migogoro ya hapa na pale na makundi yenye kuleta chuki na
kwamba mfumo wa kuteua ndiyo mfumo wa kiislam
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Halmashauri Kuu ya BAKWATA taifa Sheikh Khamis Mataka amesema mbali na
utaratibu huo wameanzisha mfumo mmoja wa kukusanya mapato ili kukusanya fedha
hizo kwa umakini tofauti na ukusanyaji wa sasa ambao una mapungufu mengi na
kupoteza baadhi ya mapato.
BAKWATA yatangaza mabadiliko ya upatikanaji wa viongozi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 05, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment