Kesi ya Aveva na Kaburu aunganishwa mwingine


Kesi inayowakabili viongozi wa juu wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Geofrey Nyange 'Kaburu' imeharishwa kwa mara nyingi tena leo hadi Aprili 12, 2018 kufuatilia ombi la upande wa mashtaka kudai wanataka kumuongeza mshtakiwa mmoja katika kesi hiyo.

Hayo yameelezwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam Thomas Simba, na Wakili wa Serikali kutoka TAKUKURU, Leornad Swai na kusema kesi hiyo ilifikishwa Mahakamani hapo kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali baada ya upelelezi wa kesi yao kukamilika.

Hata hivyo, Wakili Swai aliiomba Mahakama ahirisho fupi kwa kuwa wanatarajia kufanyia mabadiliko katika hati ya mashtaka kwa kuongeza mshtakiwa mmoja.

Kufuatia ombi hilo, Mahakama iliamua kuahirisha kesi hiyo hadi Aprili 12 mwaka 2018 kwa ajili ya upande wa mashtaka kufanya mabadiliko yao na washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Aveva na Kaburu kwa pamoja walipandishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza Juni 27 mwaka 2017 wakiwa wana kabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi ikiwemo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na utakatishaji wa fedha.

Kesi ya Aveva na Kaburu aunganishwa mwingine Kesi ya Aveva na Kaburu aunganishwa mwingine   Reviewed by KUSAGANEWS on April 05, 2018 Rating: 5

No comments: