Viongozi watatu wa Chadema wafika polisi



Viongozi watatu kati ya tisa wa Chadema tayari wamesharipoti kituo kikuu cha polisi Dar es Salaam kama walivyotakiwa kuwa wanafanya

Viongozi hao pamoja na wabunge wanaokabiliwa na mashtaka katika kesi namba 112/2018 iliyoko Mahakama ya Kisutu, wameripoti Ofisi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya masharti ya dhamana ya kesi hiyo

Ambao tayari wameshawasili ni  Katibu Mkuu, Dk Vicent Mashinji, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake(Bawacha), Halima Mdee na Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya

Viongozi hao wamekuwa wakitakiwa kuripoti polisi kama sehemu ya dhamana yao katika kesi inayowakabili polisi"
Viongozi watatu wa Chadema wafika polisi Viongozi watatu wa Chadema wafika polisi Reviewed by KUSAGANEWS on April 20, 2018 Rating: 5

No comments: