Vilio vyatawala wasanii wakimuimbia Masogange Leaders


Wasanii wameendelea kujitokeza katika shughuli ya kumuaga msanii anayepamba video za muziki ‘video queen’ Agnes Gerald, maarufu kama Masogange, huku mwanamuziki Barnaba akishindwa kuendelea kuimba na kuangua kilio

 Barnaba alikuwa akiimba wimbo wa mwanamuziki Ambwene Mwasongwe, ‘Upendo wa Kweli.’

Masogange alishiriki video ya Barnabas ya ‘Magubegube’
Kadhalika, msanii Mrisho Mpoto naye ameimba mashairi yake ambayo yamewaliza waombolezaji wengi waliojitokeza kumuaga msanii huyo

Wasanii wengine waliofika kumuaga Masogange ni Ali Kiba, Jackline Wolper, Chege, Timbulo, Kajala na Anti Ezekiel.
Vilio vyatawala wasanii wakimuimbia Masogange Leaders Vilio vyatawala wasanii wakimuimbia Masogange Leaders Reviewed by KUSAGANEWS on April 22, 2018 Rating: 5

No comments: