Wasanii wafurika kumuaga Masogange Leaders


Wasanii mbalimbali na wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wamejitokeza leo katika Viwanja vya Leaders, jijini hapa, kwa ajili ya kumuaga msanii anayepamba video za wasanii ‘video queen’ Agnes Gerald, maarufu Masogange

Mwili wa Masogange umewasili viwanjani hapa saa 11:24 asubuhi hii.

Msanii wa filamu na rafiki wa karibu wa marehemu, Irene Uwoya alibeba msalaba wakati mwili huo ukiingia Leaders.

Wasanii wengine walioonekana viwanjani hapo ni Mrisho Mpoto, Jackline Wolper, Chege, Timbulo, Kajala na Aunt Ezekiel.  

Wengine ni ‘video queen’ Tunda, msanii wa filamu, Rammy Ghalis
Mshereheshaji katika shughuli hiyo leo ni MC Pilipili
Masogange anatarajia kuzikwa kijijini kwao Utengule, Mbeya kesho.
Wasanii wafurika kumuaga Masogange Leaders Wasanii wafurika kumuaga Masogange Leaders Reviewed by KUSAGANEWS on April 22, 2018 Rating: 5

No comments: