WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ukaguzi unaofanywa kwenye
bandari ya Dar es Salaam kwa wasafiri wanaokwenda Zanzibar, hauna lengo la
kuwabagua bali ni kuimarisha ulinzi wa mipaka ya nchi.
“Hatulengi kuzuia biashara za wafanyabiashara ndogondogo, bali
tunaimarisha ukaguzi ili kuzuia wasafirishaji wa dawa za kulevya, wasambazaji
na wauzaji,” amesema.
Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Alhamisi, Aprili 19, 2018)
Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri
Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi, Bw. Jaku Hashim
Ayoub aliyetaka kupata kauli ya Serikali juu ya kuwapunguzia makali
wafanyabiashara wanaotoka Zanzibar.
Waziri Mkuu amesema: “Wanaofanya ukaguzi pale bandarini siyo
watu wa TRA peke yao kama Mheshimiwa Jaku alivyosema, bali tukumbuke kuwa
Tanzania imeingia katika vita ya dawa za kulevya, kwa hiyo tunaimarisha ulinzi
wa mipaka yetu.”
“Tanzania inapambana na matumizi ya dawa za kulevya, kwa hiyo
ukaguzi huu umelenga kuzuia watumiaji, wasambazaji na wasafirishaji wa dawa
hizo. Upekuzi huu umelenga kupunguza hili tatizo, umelenga abiria wote na siyo Wazanzibari
peke yao,” amesisitiza.
Amesema Serikali inaendelea na mipango ya kutafuta mitambo ya
kisasa ya kukagua mizigo ya wasafiri wanaotumia bandari za Tanzania bara.
Mapema, akiuliza swali lake, Mhe. Jaku alisema: “Kilio cha wabunge
wengi wanaotoka Zanzibar hapa Bungeni ni bandari ya Dar es Salaam kutoza kodi
wafanyabiashara wadogo wanaosafirisha TV au vyerehani. Ni lini utakaa nao au
kufanya ziara ya kushtukiza ili ujionee hali halisi?”
UKAGUZI BANDARINI HAULENGI KUWABAGUA WAZANZIBARI - WAZIRI MKUU
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment