Mkazi mmoja wa kijiji
na kata ya Kinaga, Kahama mkoani Shinyanga anayejulikana kwa jina la Paschal
Misana, amechunwa ngozi ya sehemu za siri na watu wasiojulikana baada ya
kuleweshwa kwa pombe.
Diwani wa kata hiyo,
Mary Manyambo amesema tukio hilo lilitokea Aprili 16, baada ya Misana kupigiwa
simu na mtu aliyekuwa akimdai Sh200,000 na watu hao kutoweka na hadi sasa
hawajajulikana walipo.
Mganga wa zamu katika
Hospitali ya Mji wa Kahama, Dk Abdallah Simba amesema kuwa mtu huyo alifikishwa
hapo juzi mchana akiwa na hali mbaya.
“Aliletwa hapa sehemu
yake ya uume ilikuwa imekatwa kwa kuzunguka na kisha kunyofolewa ngozi yote ya
sehemu hizo hali iliyosababisha kuvuja damu nyingi,” alisema.
“Wachunaji hao
walimkata kitaalamu kwani hawakufika kwenye mishipa ya sehemu za siri na hivyo
tayari ameshonwa na kurudishiwa alipokuwa amekatwa wakati wa kuchunwa.
“Sehemu zake za siri
zinaweza kuendelea kufanya kazi kama kawaida kwa sababu sehemu za mishipa
hazikukatwa.”
Akizungumzia tukio
hilo akiwa hospitalini hapo anapoendelea na matibabu, Misana alisema baada ya
kupigiwa simu hiyo alikwenda kwa lengo la kulipwa fedha alizokuwa amemkopesha
mtu huyo.
“Nilimkopesha ng’ombe
mmoja kwa thamani ya Sh200,000 na nilipofika baiskeli yangu iliingizwa chumbani
na kisha nikakaribishwa ndani,” alisema.
Misana alisema baada
ya kukaa, aliwaona wageni watatu waliokuwa chumbani, wawili wakiwa wanawake.
Alisema baadaye
alitengewa ugali ambao alikula na wenyeji na baada ya kumaliza alipewa pombe
aina ya shujaa waliyokuwa wakipewa pia wageni wengine.
Majeruhi huyo alisema
baada ya kunywa pombe hiyo alipoteza fahamu mpaka asubuhi alipozinduliwa na mke
wa mtuhumiwa.
Hata hivyo, alisema
alishangazwa na kitendo cha kuwa peke yake akiwa uchi, huku akitokwa damu na
sehemu zake za siri zikiuma.
“Sikujua chochote,
baada ya watu kujaa wasamaria wema na kuanza kunipa huduma ya kwanza,
walinieleza kuwa sehemu zangu za siri zilikuwa zimekatwa, hali iliyonishtua na
baadaye polisi walifika wakanichukua na kunipeleka hospitalini,” alisema.
Kamanda wa polisi wa mkoa,
Simon Haule alisema tayari wanamshikilia mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano.
Baada ya kuhojiwa,
mtuhumiwa huyo alisema wageni wake watatu walihusika kumchuna ngozi Misana na
kutoweka nayo na mpaka alipokamatwa hajui walielekea wapi.
Polisi wanaendelea
kuwasaka wageni hao huku mtuhumiwa akiendelea kusaidia upelelezi.
ACHUNWA NGOZI YA UUME NA WACHUNAJI WAONDOKA NAYO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment