RC MGWIRA ATOA NENO KWENYE MSIBA WA MAMA MZAZI WA RC GAMBO

Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro Anna Mgwira amewataka Vijana  kuwa na tabia  ya  kuwajali na kuwatunza wazazi wao hasa pale wanapokuwa  wagonjwa.

Mgwira ametoa rai hiyo leo wakati akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa mama  wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo Bi  Rehema  Paulo uliofanyika wilaya ya Moshi Vijijini kijiji cha Msumi mkoani Kilimanjaro ambapo amesema kuwa Vijana wanapaswa kuiga  mfano wa Gambo ambaye amemjali mama yeke hadi kufikia mauti.

Akisoma  wasifu wa marehemu  mwakilishi wa familia ya  Gambo  amesema kuwa marehemu Rehema Mumburi amefariki dunia tarehe 12 nchini India  akiwa na umri wa miaka 58 kutokana na ugonjwa wa kisukari uliokuwa ukimsumbua toka awali na baadae kuanza kusumbuliwa na figo na uvimbe uliosababisha damu kuvijia kwenye ubongo na hatimaye madaktari wakiwa wanafanya jitihada za kuokoa maisha yake aliaga dunia.

Aidha msiba huo umehudhuriwa mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, wabunge, Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini na watu wengine wengi



RC MGWIRA ATOA NENO KWENYE MSIBA WA MAMA MZAZI WA RC GAMBO RC MGWIRA ATOA NENO KWENYE MSIBA WA MAMA MZAZI WA RC GAMBO Reviewed by KUSAGANEWS on April 19, 2018 Rating: 5

No comments: