SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema Bunge haliwezi
kuidhinisha fedha kwa ajili ya matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu
Lissu kwa kuwa halijapata vibali vitatu.
Ndugai ametoa msimamo huo leo bungeni mjini Dodoma baada ya
Mbunge Godbless Lema kuomba mwongozo wa kutaka kujua sababu za Bunge
kutogharamia matibabu ya mbunge huyo wa upinzani.
Kwa mujibu wa Spika Ndugai, vibali vinavyohitajika ni pamoja na
barua kutoka kwa Rais, kibali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia
Wazee na Watoto na Hospitali ya Taifa, Muhimbili.
“Bila Bunge kupata vibali vitatu, Bunge haliwezi kuandika check
(hundi),” amesema Spika Ndugai.
Amesema, wabunge wana namna mbili ya kupata matibabu ikiwemo
kutumia kadi ya matibabu ya NHIF ndani ya nchi pekee na kutibiwa nje ya nchi
kwa vibali muhimu.
Ameushukuru Ubalozi wa Ujerumani ambao umemhakikishia kuwa ndiyo
unaofadhili matibabu ya Tundu Lissu huko Ujerumani.
“Tunawashukuru wenzetu wa Ujerumani kwa msaada wanaoutoa kumtibu
Lissu huko Ubeligiji. Nilikutana na Balozi wa Ujerumani na kunieleza hili,”
amesema.
Spika Ndugai: Tundu Lissu alikwenda kutibiwa Nairobi bila kufuata utaratibu wa Bunge
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment