Mzazi mwenzie na
msanii Alikiba Devotha ambaye amezaa naye mtoto wa kiume anayefahamika zaidi
kwa jina la Unju amefunguka mazito katika siku maalum ya msanii Alikiba ambaye
anaoa leo April 19, 2018 na kuonyesha jinsi gani yeye ametoa baraka kwa Alikiba
kuoa.
Mama Unju amesema kuwa
yeye atahudhuria katika harusi hiyo ila anakwenda kama mama wa Alikiba na kudai
kuwa msanii huyo amekuwa baba bora siku zote na kumtakia aendele hivyo hivyo
hata baada ya kuoa.
"Leo ni siku yako
maalum Kiande wangu, rafiki yangu na baba bora Alikiba, baba usiniangushe somo
yako. Mungu akusimamie katika ndoa yako. Mimi leo naenda kama Mama K, ukawe
mume bora na ujali familia zote, nenda mwanangu" alimalizia Mama Unju.
Ndoa ya msanii Alikiba
inafanyika nchini Kenya katika mji wa Mombasa leo April 19, 2016 ambapo msanii
huyo atachukua jiko lakini pia inategemewa kufanyika sherehe nyingine nchini
Tanzania siku za karibuni ndani ya mwezi huu.
Aliyezaa na Ali Kiba Afunguka Mazito
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment