WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa waache kuingilia
serikali inapotoa maagizo yenye tija kwa wananchi, likiwemo la kuwahamisha
wananchi wa mabondeni.
Majaliwa amesema, wanasiasa wanapaswa kuiunga mkono Serikali
kudhibiti maafa makubwa mvua zinaponyesha kwa wingi.
Ameeleza mikakati ya serikali kukabiliana na athari zilizotokana
na mvua zinazoendelea kunyesha ikiwemo kuagiza kamati za maafa za mikoa kufanya
tathmini ya athari hizo na mkakati wa serikali wa kujenga bonde la Msimbazi
ambalo ni chanzo cha maafa jijini Dar es Salaam.
Ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati anajibu maswali
ya papo kwa papo kutoka kwa wabunge. Wabunge walitaka serikali iainishe
mikakati ya kukabiliana na athari hasa za miundombinu zinazosababishwa na mvua
zinazoendelea kunyesha nchini.
Mbunge wa Nyang’wale Hussein Nassoro (CCM), wakati anauliza,
alieleza namna mvua zilivyoleta maafa na kubainisha kuwa takribani asilimia 75
ya miundombinu nchi nzima imeathirika, huku wananchi wakipoteza mali zao na
wengine kupoteza maisha.
“Tumepata bahati kutoka Mungu kwa mvua nyingi zinazoendelea
kunyesha lakini pamoja na hali zimekuja na maafa makubwa, je serikali
imepangaje kurejesha miundombinu hii katika hali yake ili wananchi waendelee na
shughuli za maendeleo kama kawaida?” ameuliza Mbunge huyo.
Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea (CUF), alimuuliza Waziri Mkuu
mikakati ya serikali kuhakikisha jiji la Dar es Salaam, halipatwi na maafa ya
watu kupoteza maisha na miundombinu kuharibika kila mvua zinaponyesha.
Mawaziri kujadili upatikanaji taulo za kike
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment