Kamanda wa jeshi la Polisi usalama Barabarani Mkoani
Arusha Charles Bukombe amewataka madereva wanaoendesha vyombo vya moto kuchukua
tahadhari kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha ili kuepuka madhara
yanayoweza kujitokeza.
Akizungumza na KUSAGANEWS Ofisi kwake Kamanda Bukombe
amesema kuwa madereva wasijaribu kupimo cha maji kwa kutumia gari na kuepuka
kuendesha kama wanaona kutatokea madhara.
“Madereva wawe makini wasijaribu kuyapima maji kwa
kutumia gari unapona maji ni mengi ni vema uka paki Gari ni vema ukatest wewe
kuliko ukaingiza gari “Amesema Bukombe
Pamoja na hayo amesema kuwa jeshi la polisi limejipanga
kushughulikia madereva ambao wanaenda kinyume cha utaratibu ambapo kwasasa
wanalipa faini kwa kutumia mashine kielekronic ambazo zinaonyesha taarifa za
leseni za madereva ambao hawana sifa.
“Sasa hivi adhabu zinalipwa kwa kutumia mashine za
electronic japo bado zile Manual zipo mashine zinapofeli tunatumia vitabu
lakini zile mashine zinaonyesha data halisi za madereva inavyobainika madereva
wengi wanaleseni za kufoji leseni yake class ni D ameenda sehemu akascan
wakamuongezea Class C Ukiingiza kwenye System inasoma Class D au daraja la
kuendesha pikipiki kabisa sasa niwatake tu madreva wenye leseni wanazozijua
hizo wakikamatwa watashtakiwa kwa kosa la usalama barabarani lakini watahtakiwa
kwa kosa la Fojari”Alisema Bukombe
RTO ARUSHA MADEREVA MSIJARIBU KUPIMA KINA CHA MAJI KWA KUTUMIA MAGARI YENU
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment