Spika atoa neno kwa wanawake waliotelekezwa na wabunge

Spika wa Bunge, Job Ndugai ametaka kina mama wenye malalamiko ya kutelekezewa watoto na wabunge wafike kwake au wamwandikie barua kuhusu suala hilo

Hata hivyo, amesema watakapofanya hivyo wapeleke na cheti cha uthibitisho cha vipimo vya vinasaba (DNA) ili waone ni namna gani ya kushughulikia suala hilo

Ndugai alisema hayo jana Jumanne Aprili 10, 2018 kabla ya kuahirisha kikao cha sita cha Bunge mjini Dodoma. 
Katika kauli yake iliyoambatana na vicheko Spika alisema, “Kule Dar es Salaam kuna zoezi linaendelea, huko sasa kidogo kiti cha Spika kimetikiswa hivi. Tunatuhumiwa mahali, kidogo tumeguswa hivi kwa hiyo natarajia kupata ushauri wenu waheshimiwa tunafanyaje katika mazingira haya kwa maana kuna watoto wetu wako barabarani.”
“Haiwezekani hata kidogo, kwa hiyo kina mama wale inabidi tufanye utaratibu tujue nini tutafanya lakini pia kuna kina baba wamejitokeza huko nimesikia na baadhi ya walalamikiwa ni kina mama wabunge, kwa hiyo hili jambo halina upande,” alisema Ndugai
“Hawa kina mama kama wapo, basi waje kwa spika au wamwandikie spika lakini waniletee na DNA test certificate (cheti cha uthibitisho cha vipimo vya vinasaba) ili tuone namna gani ya kuwezesha
“Kuna mafungu hapa tumepitisha tunaweza kuangalia namna ya kuweka sawasawa ili waheshimiwa wabunge wawe na utulivu katika kufanya kazi za Bunge na si kuwa na mawazo mengine,” alisema
Spika atoa neno kwa wanawake waliotelekezwa na wabunge Spika atoa neno kwa wanawake waliotelekezwa na wabunge Reviewed by KUSAGANEWS on April 11, 2018 Rating: 5

No comments: