Mbunge wa Iringa Mjini
Mchungaji Peter Msigwa amejibu tuhuma za kutelekeza mtoto, baada ya picha
kuzagaa kwenye mitandao ikimuonyesha mtoto ambaye amefanana naye akitajwa
kumtelekeza.
Akizungumza Peter Msigwa amesema
kwamba alichokiandika kwenye mitandao ya kijamii anamaanisha hivyo anamtaka
mwanamke huyo ambaye ametajwa kuwa miongoni mwa walioenda kwa mkuu wa mkoa wa
Dar e salaam Paul Makonda kwa kutelekezwa, asiishie hapo tu bali aende hata
Bungeni.
“Ilikoanzia imeanzia kwa Jerry Muro
ndiye kasambaza hizi habari, kitu ambacho nakijibu hapa amekianzisha Jerry
Muro, sasa mimi nasema kama huyo mtu yupo, nimetoa namba zangu na kama
sipatikani aje hapa Bungeni”, amesema Peter Msigwa.
Hapo jana Peter Msigwa ameandika
ujumbe kwenye ukurasa wake wa facebook akisema kwamba iwapo kweli mwanamke huyo
yupo na akithibitisha ni kweli amemtelekeza, basi yupo tayari kujiuzulu ubunge
wake alionao.
"ANAYEDAI AMEZAA NAMIMI AJE HAPA BUNGENI" MSIGWA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 11, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment