Rais Dkt. John Magufuli
amebadili maamuzi aliyotoa hivi karibuni ya kurejeshwa serikalini fedha
zilizokuwa zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Bumbuli
iliyopo wilayani Lushoto mkoani Tanga na kutaka fedha hizo ziendelee kufanya
kazi hiyo.
Rais Magufuli ametoa uamuzi huo
katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine
Shigela.
Rais Magufuli amesema kwamba
aliamuru kurejeshwa serikalini fedha zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa
jengo la Halmashauri ya Bumbuli baada ya ujenzi wa jengo hilo kutoanza kwa muda
wa miaka miwili tangu fedha hizo zitolewe hivyo alitaka kuwapa wilaya nyingine
zenye uhitaji .
Awali Rais Magufuli alifikia uamuzi
huo baada ya viongozi wa eneo hilo kutofautiana mahali pa kujenga jengo la
Halmashauri na kufanya fedha iliyotolewa na serikali kukaa bila ya kutumika kwa
zaidi ya miaka miwili.
"Halmashauri ilipitisha
kujengwa kwa Makao Makuu lakini watu wachache walikuwa wakipinga kwa ajili ya
maslahi yao binafsi. Sisi tulitoa kama Bilioni 1.3 au 4 hivi lakini fedha
zikakaa tu bila kufanya kazi. Nilitaka fedha hizo nipeleke kwenye wilaya
nyingine lakini Mkuu wa Mkoa ameniomba. Mkuu wa Mkoa amesema kwamba
mnahitaji makao makuu na ofisi nzuri. Nimebadilisha maamuzi na hizo pesa
zijenge makao makuu. Na siku nikija huko nitakuja kulitazama. Kuanzia sasa
atafutwe Mkandarasi aanze kufanya ujenzi na pesa zikipungua mniambie
nitawaongeza," Magufuli.
Pamoja na hayo Rais Magufuli amesema
kuwa siasa za kubishana bishana zimepitwa na wakati kwani Maendeleo ya
Bumbuli, Lushoto na Tanga ni ya milele sisi wanasiasa ni watu wa kupita.
Naye Mkuu wa Mkuu wa mkoa wa Tanga
ameahidi kutekeleza agizo hilo na kusema atawashughulikia wale wote
watakaojaribu kukwamisha zoezi hilo kama ilivyokuwa awali.
Raisi Magufuli abadili maamuzi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 11, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment