Mpenzi wa Nondo kunguruma mahakamani


Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Iringa inatarajiwa kusikiliza ushahidi wa anayetajwa kuwa mpenzi wa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo siku ya Aprili 18.

Upande wa Jamhuri pia inakusudia kuleta mashahidi wengine ambao ni Koplo Salum, Alphonce Mwamule, Koplo Abdulkadir na mfanyakazi kutoka Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo.

Wakili wa Serikali, Abel Mwandalamo amesema Nondo anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kusambaza taarifa za uongo akiwa Ubungo jijini Dar Es Salaam na kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari Polisi kituo cha Mafinga Wilayani Mufindi.

Wakili Mwandalamo mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya  ya Iringa John Mpitanjia, amedai upande wa Jamhuri unakusudia kuambatanisha vielelezo vya ushahidi ambavyo ni taarifa za uchunguzi kuhusiana na mawasiliano ya simu, maelezo kutoka Mjini Mafinga yakidai Nondo katekwa na kuleta kielelezo cha simu za mkononi.

Hakimu Mpita Njia ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 18, mwaka huu ambapo itaanza kusikilizwa kwa siku mbili mfululizo, kutokana na maombi ya upande wa utetezi ya Wakili Charles Luoga.



Mpenzi wa Nondo kunguruma mahakamani Mpenzi wa Nondo kunguruma mahakamani Reviewed by KUSAGANEWS on April 11, 2018 Rating: 5

No comments: