Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta amesaini muswada wa sheria ambao sasa utakuwa kamili, inayoitaka
serikali kugawa pedi bure kwa wanafunzi wa kike nchini humo.
Rais Kenyatta amesaini sheria hiyo
jana Aprili 10, ambayo pia inaitaka serikali kuweka mazingira salama kwa
wanafunzi hao kuweza kuhifadhi pedi zao.
“Sheria ya Marekebisho ya Elimu ya
Msingi, kuweka wajibu wa kutoa taulo za usafi (pedi) za kutosha na za ubora kwa
kila mtoto msichana aliyesajiliwa na kujiandikisha katika taasisi ya elimu ya
msingi ya umma na kufikia ujira, kwa serikali”, imesema taarifa iliyotolewa na
serikali ya Kenya kwa vyombo vya habari.
Ripoti ya UNESCO ya mwaka 2016
imeeleza kwamba binti mmoja kati ya 10 kwenye nchi zilizopo kusini mwa jangwa
la Sahara, anakosekana shuleni kwa siku ambazo yupo kwenye hedhi, kutokana na
kukosa pedi za kujistiri.
Rais Kenyata asaini sheria ya pedi bure kwa wanafunzi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 11, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment