Mbunge wa Ulanga (CCM), Gudluck Mlinga
ameomba mwongozo wa Spika bungeni akitaka kujua namna chombo hicho cha Dola
kinavyoweza kuzuia wanawake waliofika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda kwa madai ya kutelekezwa na watoto wao
Mlinga ameomba mwongozo huo leo Jumatano
Aprili 11, 2018 akisema kitendo hicho kinawadhalilisha watoto ambao hufika
katika eneo hilo wakiwa na mama zao, akidai kuwa kinavunja Katiba ya nchi
Mwongozo huo uliibua kelele bungeni baada ya
mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga kutoa majibu kwamba suala hilo ni la kisheria,
kupingwa na wabunge waliohoji sheria ipi
Mlinga alitaka kujua namna ambavyo Makonda
anavyovunja Katiba kwa kuanika mambo ya siri hadharani jambo ambalo linakwenda
kinyume na Katiba, akitaka Bunge liingilie kati na kukemea kitendo hicho
Mlinga ataka utaratibu wa Makonda usitishwe mara moja
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 11, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment