Serikali ya awamu tano
kupitia Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametoa mwezi mmoja kwa mameneja
wote wa mikoa wa Shirika la Umeme nchini Tanesco kuwaunganishia umeme wananchi
ambao tayari washalipia huduma hiyo na meneja atakayeshindwa kutekeleza agizo
hilo ajiuzulu kazi mara moja.
Dkt. Kalemani ametoa agizo hilo
wakati alipokuwa kwenye ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya
usambazaji wa umeme vijijini (REA), awamu ya tatu katika maeneo mbalimbali
wilayani kyela na kusema wananchi wamekuwa wanaolipia huduma ya kuunganishiwa umeme
wamekuwa wakipatia kero nyingi bila ya kupewa huduma hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Hunter Mwakifuna ameishukuru Wizara ya Nishati
kuwa kuwaelekeza wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini kuwashirikisha
viongozi wa maeneo husika, hatua ambayo imepunguza malalamiko kutoka kwa
wananchi.
SerikaliYATOA siku 30 Kwa TANESCO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment