Serikali yafanikiwa baada ya kuweka mikakati hii


Serikali imesema,  imefanikisha kuyashughulikia matukio 1,072  kwa mwaka 2017 yaliyoripitiwa kupita namba maalum iliyotolewa na Serikali kwa ajili ya kuripoti matukio ya udhalilishaji na unyanyasi hususan Wanawake na Watoto.

Akizungumza leo Bungeni Mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto,  Dk. Faustine Ndugulile, amesema hiyo ni kati ya mikakati mingi iliyowekwa na serikali kwa ajili ya kukomesha matukio ya udhalilishaji kwa watoto nchini.

Aidha, Dk. Ndungulile amesema,  Wizara yake  tayari imeshatoa mafunzo kwa Maafisaa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii wapatao 50 katika mikoa yote 26 kwa ajili ya kuanzisha Kamati za Ulinzi kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa ili kupunguza kama si kumaliza kabisa tatizo hilo.

Serikali yafanikiwa baada ya kuweka mikakati hii Serikali yafanikiwa baada ya kuweka mikakati hii Reviewed by KUSAGANEWS on April 05, 2018 Rating: 5

No comments: