Mwandishi Wetu,Arusha
Mkuu wa mkoa Arusha,Mrisho Gambo ameagiza halmashauri zote za mkoa
Arusha kupanda miti 1.5 milioni kwa mwaka ili kutunza mazingira.
Gambo alitoa hutuba hiyo kwenye maadhimisho ya upandaji miti mkoa
Arusha ambayo yalifanyika kijiji cha Selela wilaya ya Monduli.
Katika hutuba ya Gambo ambayo ilisimwa na Mkuu wa Wilaya ya
Karatu,Theresia Muhonga alisema ili kufanikisha hilo,kila halmashauri inapaswa
kutenga fedha kila mwaka.
"Tengeni fedha kila mwaka kusaidia kupanda miti na
kuihifadhi" alisema
Mkuu huyo wa mkoa alizitaka halmashauri kushirikiana na wadau
mbali mbali ili kufanikisha hilo zikiwepo sekta binafsi.
Awali Meneja Masoko wa kampuni ya Mobisol,David Ngwale ambao
walikuwa sehemu ya wadhamini wa zoezi hilo,alisema suala la utunzwaji mazingira
ni la watanzania wote.
Alisema kampuni yao ambayo huzalisha umeme wa jua itaendelea
kusambaza huduma huyo hasa maeneo ya vijijini ili kuzuia uharibifu wa mazingira
katika kupata nishati ya umeme.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Monduli,Stivin Ulaya alisema wilaya
hiyo kwa kushirikiana na wadau ikiwepo Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro
imejopanga kukabiliana na uharibifu wa mazingira.
"Tumekuwa na miradi ya kupanda miti,kuhimiza majiko sanifu na
tunashukuru wadau kama Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro kusaidia" alisema.
Meneja wa malisho ya wanyama katika mamlaka ya hifadhi ya
Ngorongoro, Hillal Mushi alisema Mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na
serikali misitu na kulinda vyanzo vya maji.
Alisema NCAA pia imekuwa na miradi ya kusambaza miti bure vijijini
ili kuhakikisha mazingira yanatunzwa kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.
Mwisho.
Rc Arusha aagiza kila halmashauri Arusha kupanda miti 1.5 kwa Mwaka
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 08, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment