Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dokta John Magufuli
amesema mahuburi na mafundisho yanayotolea makanisani na misikitini
yanarahisisha utendaji kazi wa serikali hivyo ataendelea kushirikiana na
madhehebu yote dini katika nyanja zote.
Rais Magufuli amesema hayo jana
alipohudhuria ibada ya kuapishwa kwa askofu Mkuu wa Jimbo kuu Katoliki
Arusha ambapo ameeleza kuwa madhehebu ya dini yamekuwa yakihubiri amani
kwakuwa amani ni muhimu katika maisha ya kila Mtanzania hivyo ata endelea
kushirikiana na madhebu yote ya dini ili kuijenga amani ya nchi.
Aidha Rais Magufuli akijibu
yaliyotolewa na umoja wa mapadri wa Jimbo kuu Katoliki Arusha juu
ya kuhamishwa kwa shule ya msingi Naura iliyopo katika eneo la
kanisa,kumilikishwa bustani ya naura iliyo mbele ya kanisa hilo pamoja na
kusamehewa kodi inayodaiwa na serikali kwa shule ya st Judi inayomilikiwa
na kanisa hilo amesema kuwa atakaa na serikali kuona ni yapi watanya atakama ni
ushauri tuu mambo yote yapo kisheria na huwezi kutoa maamuzi yatakayoweza
kuleta mgogoro katika nchi.
mhashamu askofu Mkuu wa Jimbo
Katoliki Arusha ambaye ndiye aliyeapishwa Askofu Isac Amani amesema Siasa safi
ni ile inayounganisha vyama vyote kuwa pamoja na kuweza kufanya kazi za
maendeleo kwa kushirikiana hivyo wasirujusu ufa utaoweza kuharibu ustawi
wa nchi.
RAISI MAGUFULI AAHIDI KUSHIRIKANA NA MADHEHEBU YOTE YA DINI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 08, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment