Raisi Magufuli atoboa Siri ya Yeye na Mkewe

Rais John Magufuli leo ametoboa siri kuwa mke wake, Janeth alikuwa ni mtoto wa polisi

Ameyasema hayo leo Aprili 7 wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za polisi  mjini Arusha na kusema baba mkwe wake alikuwa sajenti wa polisi

“Nyumba za polisi ndizo zimenipa mke kwa hiyo nyumba za polisi ninazifahamu, huyu mke wangu niliye naye alikuwa mtoto wa polisi, marehemu baba yake hakuwa na cheo kikubwa alifariki akiwa sajenti,” amesema

Ameongeza kuwa, “Ingekuwa nazindua Moshi, angenionyesha nyumba walizokaa lakini za Oysterbay alizoishi alishanionyesha na za Ukonga na za sehemu nyingine. Kwa hiyo maisha ya polisi ninayafahamu.”
Amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kuhakikisha polisi hao wanaingia kwenye nyumba zao kesho.
Raisi Magufuli atoboa Siri ya Yeye na Mkewe Raisi Magufuli atoboa Siri ya Yeye na Mkewe Reviewed by KUSAGANEWS on April 07, 2018 Rating: 5

No comments: