Raisi Magufuli Ampongeza Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha

Raisi Dkt John Pombe Magufuli Amempongeza meya wa Jiji la Arusha Ndugu Kalist Lazaro kwa kazi nzuri anayoifanya katika jiji hilo.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akihutubia mamia ya wakazi wa Jiji hilo katika maonyesho hayo yaliyoenda sanjari na maandimisho ya miaka 46  ya kumbukumbu ya kifo cha Hayati Amani Abeid Karume .

Rais Magufuli amesema Meya hiyo amekuwa na desturi ya kumpokea kila anapokuwa kwenye ziara zake mkoani hapa na hivyo hana itikadi za kisiasa ila Moyo wake ni kuchapa kazi.

"Kwenye maendeleo hapahitaji siasa ndio maana hata Meya wa hapa amekuwa akinipokea kila nikija Hapa Kwa sababu anachapa kazi bila kujali vyama" Amesema Magufuli.

Rais Magufuli Alimwita  Meya huyo aliyekuwa ameketi kiti cha Nyuma katika jukwaa kuu na Kumtaka aje mbele ili aketi mahala alipo na alipofika alimshika mkono na kuuinua juu huku akisema kuwa...... huyu ni kiongozi mchapa kazi asiyejali itikadi za vyama

"Si mmemwona.... huyu Meya ni mchapa kazi kweli kweli haangalii vyama"

Raisi Magufuli Ampongeza Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Raisi Magufuli Ampongeza Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Reviewed by KUSAGANEWS on April 07, 2018 Rating: 5

No comments: