Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini (IGP) Simon Sirro amesema Jeshi lake liko imara kweli kweli katika
kupambana na watu wanaotaka kuleta uvunjifu wa amani nchini, huku akiwasii
wanaotaka kuandamana kuacha mara moja kwani kitakachowapata wasije kulaumiana
IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo
(Aprili 7, 2018) wakati akitoa salamu zake kwa Rais Dkt. Magufuli katika uwanja
wa Sheikh Amri Abeid uliopo mjini Arusha baada ya uzinduzi wa nyumba za askari
na kushuhudia maonesho ya utayari ya jeshi hilo katika kukabiliana na uhalifu.
"Mhe. Rais Magufuli Jeshi lako
Polisi liko imara tena imara kweli kweli, kwa kupambana na watu wote wanaotaka
kuleta uvunjifu wa amani hapa nchini na kwa bahati nzuri wananchi wapo pamoja
na wewe Rais na Jeshi lako. ila naomba nitoe ushauri wa bure kwa wale wote
wenye nia ya kuchafua amani ya nchi yetu , ni wasii waache mara moja na kama
wataona ushauri huo hauna maana basi baadae tusilaumiane", amesema IGP Sirro.
Pamoja na hayo, IGP Sirro ameendelea
kwa kusema "upo uhamasishaji kwenye mitandao, na hili niseme
naamini wameshaandamana kwenye mitandao na wameshamaliza maandamano yao.
Kwa hiyo la msingi sana tujenge nchi yetu".
Kwa upande mwingine, IGP Sirro
amesema katika kipindi cha mwezi Januari hadi Februari mwaka 2018 kuna jumla ya
matukio ya jinai yaliyoripotiwa ni 96,363 ikilinganishwa na matukio 104,073
yaliyoripotiwa kipindi kama hicho mwaka 2017.
IGP Sirro atoa maelekezo kwa wanaotaka kuandamana
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 07, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment