Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko na
masikitiko makubwa taarifa ajali iliyotokea usiku wa jana Mkoani Tabora na
kusababisha vifo vya takribani watu 12.
Dkt. Magufuli ameeleza hayo kwenye
salamu zake za rambirambi alizozitoa leo Aprili 05, 2018 baada ya kupita siku
moja tokea basi la kampuni ya City Boy lililokuwa limebeba abiria kutoka
Karagwe Mkoani Kagera kuelekea Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na lori aina
ya Fuso lililokuwa linatoka Singida kuelekea Igunga.
“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko
makubwa taarifa ya vifo vya watu 12 waliopoteza maisha katika ajali ya
barabarani iliyotokea jana usiku katika wilaya ya Igunga mkoani Tabora, nawapa
pole wafiwa wote, ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu mkubwa.
Nalitaka Jeshi la Polisi, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya na
Mamlaka zote zinazohusika na usalama wa barabarani kujitathmini, na kutafuta
majawabu ya kwa nini ajali za barabarani zinaendelea kutokea kwa kusababishwa
na uzembe na uvunjaji wa sheria za barabarani?”, amesema Dkt. Magufuli.
Pamoja na kutoa pole kwa wafiwa,
Dkt. Magufuli amewataka viongozi wote wanaohusika na usimamizi wa usalama wa
barabarani kutafakari kwa nini ajali nyingi zimekuwa zikitokea katika maeneo
yaleyale na kutafuta ufumbuzi ili kuepusha madhara ya watu kupoteza maisha,
kupata ulemavu wa kudumu na kupoteza mali.
Kwa habari kamili soma hapa chini.
Rais Magufuli asikitishwa na vifo, atoa agizo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 05, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment