Mbunge wa Tarime vijijini, John Heche
ameunganishwa katika kesi inayowakabili viongozi saba wa Chadema na
kusomewa mashtaka matatu ikiwamo kuchochea chuki
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya jinai
namba 112 ya 2018 ni Mwenyekiti wa Chadema, Taifa, Freeman Mbowe, Mbunge wa
Iringa Mjini Peter Msigwa na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu
Wengine ni Naibu katibu Mkuu bara,
John Mnyika, Mbunge wa Tarime mjini Ester Matiko, Katibu wa chama hicho Dk
Vincent Mashinji na Halima Mdee Mbunge wa Kawe
Hata hivyo baada ya kusomewa mashtaka hayo
Heche alifanikiwa kupata dhama
Akimsomea mashtaka, Heche, Wakili wa
Serikali Mkuu Faraja nchimbi alidai kuwa Heche na wenzake hao saba kwa pamoja
walitenda makosa hayo Februari 16, 2018 maeneo ya Viwanja vya Buibui na
barabara ya Kawawa wilayani Kinondoni, Dar es Salaam
shtaka la kwanza Heche anadaiwa kufanya
mkusanyiko usio halali kinyume na sheria, katika barabara ya Kawawa Mkwajuni
wilayani Kinondoni Dar es Salaam, Februari 16.
Shtaka la pili ni kuendelea kufanya
mkusanyiko usio halali, licha ya kutakiwa kuondoka eneo hilo na Ofisa polis
Gerald Ngiichi na hivyo kusababisha kifo cha Akwilina Akwilini. Huku askari
wawili wakijeruhiwa katika mkusanyiko huo.
Shtaka la tatu, linamkabili
Heche peke yake ambapo, anadaiwa kuwa Februari 16, mwaka huu katika
viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, alihutubia katika
mkutano wa hadhara na alitamka maneno yenye kuchochea chuki akisema
“Kesho patachimbika, upumbavu unaofanywa
kwenye nchi hii...wizi...unaofanywa na Serikali ya awamu ya tano...watu
wanapotea...watu wanauawa wanaokotwa kwenye mitaro lazima ukome."
Nchimbi alidai kuwa maneno hayo yalielekea
kuleta chuki na manung'uniko miongoni mwa jamii na wakazi wa Tanzania
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Heche
alikana na Aprili 16, 2018 yeye na wenzake saba watasomewa maelezo ya awali
mahakamani hapo
Heche aliachiwa kwa dhamana baada ya
kukamilisha masharti ya dhamana, ya kuwa na wadhamini wawili wenye barua za
viongozi wa mtaa, vijiji ama waajiri wao na nakala za vitambulisho vyao.
Kama ilivyokuwa kwa kina Mbowe, wadhamini
hao kila mmoja atasaini bondi ya Sh 20 milioni na mshtakiwa kuripoti polisi
kila Alhamisi.
Makosa matatu ya Heche haya hapa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 05, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment