Msanii wa nyimbo za
Injili nchini, Emmanuel Mbasha amesema amesikitishwa na taarifa alizozipata
kuwa amempa ujauzito msichana anayevuma kwenye mitandao ya kijamii Agness na
kudai hana mahusiano yeyote na mtu huyo zaidi ya kumfahamu kupitia mitandaoni
Mbasha amebainisha hayo kupitia
kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana baada ya kuwepo
na tetesi za muda mrefu zinazozidi kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa
zinadai kuwa wawili hao wana mahusiano ya kimapenzi na mpaka kufikia hatua ya
kukubalia kupeana ujauzito.
"Agness mimi namfahamu kama
shabiki yangu kupitia mitandao ya kijamii. Sasa sielewi mambo yamegeuka vipi
mpaka kufikia hatua ya kuambiwa mimi nina mahusiano naye. Sijawahi kuwa na
mahusiano na Agness na wala sijawahi kuwa na chochote kile kinachoashiria
mapenzi", amesema Mbasha.
Pamoja na hayo, Mbasa ameendelea kwa
kusema "sitegemei kupata naye mtoto kama watu wanavyosema kwa
kuwa sina mahusiano nae kwa vyovyote vile huyo msichana ni shabiki wangu
tu".
Mbasha Sijampa mimba Agness
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 05, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment