Rais John Magufuli ametuma salamu za
rambirambi za kifo cha mkuu wa mkoa mstaafu, Abbas Kandoro akisema Taifa
limepoteza mtu muhimu ambaye mchango wake hautasahaulika
Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano
ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa aliyoitoa leo Aprili 28, 2018 amesema Rais
Magufuli Kandoro alikuwa kiongozi shupavu, aliyejiamini na kutekeleza majukumu
yake kwa kuzingatia sheria na taratibu, aliwapenda watu aliowaongoza na
alidhirisha uzalendo wa kweli
Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Mkoa
wa Iringa, Amina Masenza kufikisha salamu hizo kwa familia ya marehemu, ndugu,
jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huo.
“Nimesikitishwa
sana na kifo chake, nawaombea wafiwa wote wawe na moyo wa subira, uvumilivu na
ustahilivu katika kipindi hiki cha majonzi na pia namuombea marehemu Abbas
Kandoro apumzike mahali pema peponi, Amina,” amesema Rais Magufuli
Enzi za utumishi wake, Kandoro
amehudumu mikoa ya Tabora, Arusha, Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya
Kandoro alifariki jana Aprili 27,
2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na anatarajiwa kuzikwa kesho
Aprili 29, 2018 mkoani Iringa
Rais Magufuli amlilia Abbas Kandoro
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 28, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 28, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment