Mbunge wa Tarime
Vijijini, John Heche amefunguka kuwa mpaka sasa haelewi ni kwa vipi mtu anaweza
kuuwawa na polisi kwa kuchomwa kisu tena akiwa amefungwa pingu huku
akikumbushia tukio la mdogo wake mwingine kujeruhiwa vibaya na polisi ambapo
alisababishiwa ulemavu mwaka jana.
Mbunge Heche amesema kwamba mtu
kuchomwa kisu mgongoni ni kudhamiria kuua kwasababu mtu huyo hakuwa
anapambana.
"Nilijua mikononi mwa polisi ni
sehemu salama, wiki mbili zilizopita kijana Allen alikufa katika mazingira tata
kule Mbeya, Mwanza mama aliyekamatwa na kunyimwa dhamana mtoto wake mchanga
alikufa. Leo ni kwangu mdogo wangu ameuwawa kikatili sana mikononi mwa polisi.
Maisha yangu yote nimeyatoa kupigania haki ili watu wasionewe, mtuhumiwa
asifanywe mkosaji na kuhukumiwa kabla ya vyombo vya sheria kumhukumu,"
Heche.
Ameongeza " Mwaka jana mdogo
wangu mwingine aliumizwa vibaya sana na polisi. IGP Mangu na RPC waliokuwa
Tarime walilipa uzito suala hilo lakini walipoondolewa, suala liligeuzwa
kisiasa na wale vijana waliokua wamemjeruhi mdogo wangu ambaye mpaka sasa sikio
moja halisikii,wakarudishwa kazini kinyemera na kuhamishwa Tarime kama
kunikomoa. Mimi nimewahi kutishiwa kuuwawa kituo cha polisi, najisikia maumivu
makubwa mno lazima Watanzania wakatae hali hii".
Pamoja na hayo Mbunge huyo amehoji
juu ya ukimya wa Waziri na kuongeza kwamba ni watu wangapi wanakufa na kuumizwa
mikononi mwa polisi bila matukio kujulikana wala kutangazwa na kuweka wazi
kwamba atazungumza muda ukifika.
Heche atoa ya moyoni baada ya kifo cha Mdogo wake
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 28, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 28, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment