Misungwi. Ofisa Mifugo wa Wilaya ya
Nyamagana jijini Mwanza, Michael Fundo (57), amefariki dunia kwa kunywa sumu
kabla ya kujitundika kwa kamba ndani ya zizi la ng’ombe nyumbani kwake wilayani
Misungwi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,
Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo linalodaiwa kusababishwa na
msongo wa mawazo kutokana na Michael kuwa na ugomvi wa muda mrefu wa kifamilia
Mmoja wa wanafamilia aliyezungumza
kwa sharti la kutotajwa jina, amesema ugomvi huo ulitingisha pia ndoa yake
“Kabla ya kujinyonga kwa kamba,
alikunywa sumu aliyoona inamchelewesha,” amesema Kamanda Msangi
Licha ya kuwa mtumishi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Nyamagana ambayo kwa pamoja na Ilemela zinaunda Jiji
la Mwanza, Michael alikuwa akiishi wilaya jirani ya Misungwi
Mtumishi wa ndani wa familia hiyo,
John Anthony (23) amesema kabla ya kuchukua uamuzi wa kujitoa uhai, alifanya
hesabu ya kikundi cha kuweka na kukopa ambacho alikuwa mtunza fedha na
kukabidhi nyaraka na fedha zote akielekeza zikabidhiwe kwa wana kikundi wenzake
“Marehemu pia aliandika wasia
ukihusisha mali pamoja na madeni anayodai na kudaiwa, jambo lililotutia mashaka
ni kwa nini anafanya hivyo,” amesema Anthony
Ofisa mifugo ajiua kwa kujitundika kamba kwenye zizi la Ng"ombe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 28, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 28, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment