Jeshi la Polisi mkoani
Lindi, limemtimua kazi askari wake wa kituo cha wilaya ya Ruangwa, H.1302
Bariki Michael {28} kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 14 (Jina
limehifadhiwa kwa maadili).
Hayo yameelezwa na Kaimu Kamanda wa
Jeshi hilo mkoani hapa, SSP Renatu Chalya alipokuwa anazungumza na mwandishi wa
habari Ofisini kwake na kusema mtuhumiwa huyo tayari amefikishwa Mahakamani
akikabiliwa na Shitaka hilo, na kwa sasa yupo mahabusu akikabiliwa na shitaka
hilo.
"Tayari tumeshamaliziana na
askari Bariki Michael kwa kumtimua kazi ndani ya Jeshi. Unajuwa Jeshi letu la
Polisi halitetei na kulea askari wasio na nidhamu", amesema Kaimu Kamanda Chalya.
Kwa upande mwingine, Kaimu Kamanda
Chalya amesema mtuhumiwa huyo atapandishwa tena Mahakamani mnamo Aprili 14,
2018 ili aweze kusomewa shitaka linalomkabiri dhidi yake.
Polisi atimuliwa kazi kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 14
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 06, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment