Mbunge wa Kigoma Mjini
kupitia ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa yupo tayari
kukamatwa na polisi lakini pia yupo tayari hata kuuwawa kwa ajili ya kuisemea
trilioni 1.5 ambayo CAG amesema haijatolewa maelezo imetumikaje.
Zitto Kabwe amesema hayo leo April
18, 2018 baada ya Katibu Mwenezi wa CCM Humphrey Polepole kusema kuwa wapo
viongozi wa upinzani wanasema uongo juu ya ripoti Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) na kutaka watu hao wachukuliwe hatua. Kufuatia kauli
hiyo Zitto Kabwe amesema kuwa anauhakika kuwa serikali ya awamu ya tano
imeshindwa kuonyesha matumizi ya trilioni moja na bilioni mia tano.
"Kuna mtu anasema nikamatwe kwa
kupotosha Kuhusu TZS 1.5trn zinazohojiwa na CAG. Mimi Kabwe Zuberi Ruyagwa
Zitto, Mwenyeji wa Kigoma, Muislam, naapa kwamba Serikali ya CCM ya awamu ya
tano imeshindwa kuonyesha kwa CAG matumizi ya shilingi trilioni moja na bilioni
mia tano. Nipo tayari kukamatwa kwa kusema hivyo ( haitafuta ukweli wa
ubadhirifu huo"
Aidha Zitto Kabwe amekwenda mbali na
kusema kuwa yupo tayari hata kufa kwa kuwa anaamini mawazo yake hayawezi kufa
hata kidogo "nipo tayari kuuwawa kwa kusema hivyo kwani mawazo
yangu hayatakufa. Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie" alisisitiza
Zitto Kabwe
Mwisho wa wiki iliyopita, Mbunge wa
Kigoma Mjini kwa triketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe aliizungumzia kwa mapana
zaidi taarifa ya CAG na kuonyesha mambo ambayo serikali imetuhumiwa kufanya
ikiwa pamoja na upotevu wa fedha zaidi ya Trilioni 1.5 ambayo haina maelezo
imetumikaje.
Nipo tayari kuuwawa kwa trilioni 1.5 - Zitto Kabwe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 18, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment