Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema ili
mbunge aweze kutibiwa nje ya nchi kwa gharama za Bunge anapaswa kuwa na vibali
vitatu; kibali cha Bunge, Hospitali ya Taifa Muhimbili na Rais John Magufuli
Ametoa kauli hiyo wakati akijibu mwongozo wa
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema aliyehoji sababu za Bunge
kushindwa kutoa gharama za matibabu za mbunge wa chama hicho Singida Mashariki,
Tundu Lissu
"Kuna siku nitataja orodha ya wabunge
wanaotibiwa nje ya nchi. Ni lazima wawe na vibali hivi. Rais alishasema wazi
kuwa anazuia safari za nje zisizokuwa na lazima. Lissu alipelekwa Nairobi
katika matibabu kwa utaratibu ambao haukuwa na kibali cha Bunge. Hili jambo
nimeshalisema sana sijui kwanini linajirudia, "amesema na kuongeza
Spika: Lissu alikwenda kutibiwa Nairobi bila kufuata utaratibu wa Bunge
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment