Meneja wa Fedha wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) afikishwa Mahakamani kwa kumiliki Nyumba 23, Magari 7
Leo April 19, 2018
Meneja wa Fedha wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Prosper Kimaro
amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la
kujilimbikizia mali zenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.4 zisizolingana na
kipato chake halali.
Kimaro anadaiwa
kumiliki nyumba zenye thamani ya Bilioni 1,178,370,334, zilizopo maeneo ya
Temeke DSM na magari 7 yenye thamani Shilingi Milioni 307,364,678.20.
Kimaro amesomewa mashtaka
yake na wakili wa serikali, Vitalis Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas
Simba ambapo amedai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja.
Wakili Vitalis amedai
mshtakiwa anakabiliwa na kosa la kujilimbikizia mali zisizolingana na kipato
chake ambapo anadaiwa amelitenda kosa hilo kwa miaka tofauti kati ya 2012 na
2016.
Anadaiwa mali hizo
amejilimbikizia maeneo ya Temeke DSM akiwa mtumishi wa umma wa TPA kama Meneja
wa Fedha, amekutwa na mali zisizolingana na kipato chake halali cha zamani na
cha sasa.
Mali hizo ni nyumba 2
zilizopo mtaa wa Uwazi Temeke (Mil 124.2), kiwanja kimoja kilichopo Yombo
Vituka (Mil.12.9), nyumba 2 zilizopo Temeke (Mil 63.5).
Pia nyumba nyingine 3
zilizopo Temeke zenye thamani ya (Mil.159), nyumba nyingine 3 zilizopo maeneo
hayo (Mil 170.1), nyumba nyingine moja (Mil 71.3).
Pia ana kiwanja Temeke
(Mil 35), kiwanja kingine (Mil 25) na kujenga nyumba 3 (Mil 159), pia nyumba
nyingine moja (Mil 106), pia nyumba nyingine 3 zilizopo Temeke zikiwa na
thamani ya (Mil 214).
Pia ana nyumba 4
zilizopo Viziwa Ziwa Kibaha Mjini (Mil 199.7), nyumba nyingine Kilimahewa
Tandika (Mil 70).
Pia anamiliki magari
aina ya Toyota Land cruise (Mil 180.1), Mitsubishi (Mil 38.4), Massey Ferguson
(Mil.24), Trailer (Mil 4.5), Toyota Harrier (Mil 35.8), Trailer (Mil 4.8),
Massey Ferguson (Mil 19.1).
Baada ya kusomewa
mashtaka hayo, mshtakiwa alikana makosa yake ambapo Wakili Vitalis amedai
upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, pia hana pingamizi na dhamana.
Hakimu Simba ametoa
masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini 2 watakaowasilisha hati ya
mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh.Mil 200, pia mshtakiwa asitoke nje ya
mkoa wa Dar es Salaam bila kibali pamoja na kuwasilisha hati zake za kusafiria.
Mshtakiwa huyo
hajatimiza masharti ya dhamana, ambapo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi
May 3,2018.
Meneja wa Fedha wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) afikishwa Mahakamani kwa kumiliki Nyumba 23, Magari 7
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment