Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wale wote wanaosema kampeni yake
ya kuwasaidia akina mama waliotelekezwa na watoto imevunja sheria, pengine wana
watoto nje na wanaogopa kujitokeza.
Makonda ameyasema hayo
leo Aprili 19, katika uzinduzi wa hospitali ya kisasa ya mama na mtoto iliyopo
Chanika iliyojengwa kwa msaada wa Shirika Maendeleo la Kimataida la Korea
(Koica).
“Eti wanasema navunja
sheria, natakiwa nifanye faragha kama unataka faragha tunza mtoto. Mimi
siogopi, nipo tayari kufungwa lakini kwa ajili wa kutetea haki za watoto.
Pengine hao wanaosema navunja sheria wana watoto wao nje wanaogopa kujitokeza,”
amesema.
Jana, Waziri wa Sheria
na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi akiwa bungeni alisema kampeni hiyo
inaweza kuleta hali ya sintofahamu na akabainisha kuwa inapaswa kufanyika
faragha na sio kama inavyofanyika sasa.
Awali, Waziri wa Afya,
Jinsia, Wanawake na Watoto, Ummy Mwalimu alisema kampeni hiyo ni sahihi
ila kasoro yake ni kutokuwa na faragha, lakini akasema kwa sasa inafanyika huku
picha za watoto zikifichwa.
Aliyeibua hilo bungeni
jana alikuwa ni mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliyehoji uhalali wa kampeni
hiyo na akahoji kama haivunji sheria na kuwavunjia haki wanawake na watoto.
Makonda awajibu mawaziri Waliompinga Jana
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment