Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Usharika wa Kigogo, Richard Hananja amedai kuna ubabe katika kanisa
hilo
Hata hivyo, amesema licha ya kanisa hilo kupitia mambo mengi
anaamini litaendelea kusimama imara hasa katika kipindi hiki
Mchungaji Hananja amesema hayo Aprili 29, 2018 alipozungumza
na Mwananchi kuhusu baraza la maaskofu wa KKKT ‘kuwatenga’ maaskofu watatu kwa
kutosoma waraka wa ujumbe wa Pasaka kwenye dayosisi zao
Amedai kuna ukabila na makundi, huku watu wakichukuliwa
hatua kibabe kwa mambo yanayotokea hata kama hawakuhusika
“Kwenye haya makanisa kuna ubabe mkubwa, kuna ukabila na
makundi. Ninyi wa nje hamuwezi kuona, sisi wengine tulishafukuzwa muda mrefu
lakini bado tupo kwa sababu,” amedai
Amesema kanisa ni taasisi inayohubiri amani na iwapo
maaskofu wameona wamtenge mwenzao hilo ni la kwao
“Yale unayomtendea mwenzio ndiyo utakayotendewa,” amesema
Mchungaji Hananja.
Mchungaji KKKT atoa neno uamuzi wa maaskofu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 30, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 30, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment