Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka
25 ambaye ni raia wa Afrika Kusini, amehukumiwa kwenda jela maisha kwa kosa la
kumlinda mbakaji wa mtoto wake mwenye umri wa miezi miwili, na mahakama kuu ya
Johanesburg.
Mwanamke huyo ambaye hajatajwa jina
kwa ajili ya kulinda utambulisho wa mtoto wake, alikuwa akikanusha taarifa ya
daktari na kile kilichoaminiwa na mahakama baada ya mtoto wake wa miezi miwili
kuonekana amebakwa na kuumizwa vibaya.
Mama huyo amekuwa akisema mtoto wake
hajabakwa isipokuwa ameanguka wakati akiwa amelala na kuangukia goti lake, na
ndipo alipoumia.
Lakini hata hivyo mahakama ilimbana
mwanamke huyo kwa kumuuliza kama alinguka na hakubakwa majeraha ya ndani na
mbegu za kiume alizitoa wapi, na kushindwa kujibu huku akisisitiza hajabakwa na
mtu yeyote.
“Mtuhumiwa anashindwa kuelezea ni
kwa namna gani mtoto ameumia kwa ndani na sio nje, na ushahidi unaonyesha
sehemu za kiume ziliingia ndani ya sehemu za siri za mtoto na kumjeruhi
(kumpasua), namna pekee ambayo tunaweza kujua ni namna gani ilitokea, ni yeye
pekee ndiye anayejua”alisikika Jaji Veenendal Said.
Mahakama ya Afrika Kusini ilikuwa
inamtaka mama huyo kumtaja mtu aliyemfanyia kitendo hiko cha ukatili mtoto huyo
ambaye memzaa mwenyewe, na kueleza kilichotokea, lakini mwanamke huyo kukataa
kata kata, na mahakama kushwangazwa ni kwa nini hataki kusema ukweli na
kumhukumu kwenda jela maisha.
Taarifa zinasema kwamba mwanamke
huyo ameolewa na amekuwa akiishi kwenye ndoa yenye manyanyaso na vipigo kutoka
kwa mume wake, na hata alipokuwa kwenye kesi mume wake huyo hakuja kumtembelea
wala kumletea mahitaji yoyote ya msingi, tangu Novemba 2016 ambapo tukio hilo
la ubakaji lilitokea.
Mama afungwa maisha kwa kumlinda mbakaji
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 12, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment