Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anaondoka leo Aprili 15, 2018
kwenda jijini London nchini Uingereza kumwakilisha Rais John Magufuli
katika mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola (CHOGM
Mkutano huo utafanyika kuanza kesho, Aprili 16 hadi 20 na
utafunguliwa na Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Malkia Elizabeth wa
Pili wa Uingereza ukiwa na kaulimbiu inayosema, “Kuelekea
mustakabali wa pamoja” na utaongozwa Waziri Mkuu wa Uingereza,
Theresa May atakayekuwa mwenyekiti.
Taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya Makamu wa Rais imesema
majadiliano ya mkutano huo yatajikita kwenye maeneo manne
makuu ya kipaumbele ambayo yatajadili namna ambavyo Jumuiya ya
Madola inaweza kufikia mustakabali wenye ustawi zaidi; mustakabali
endelevu zaidi; mustakabali wenye haki zaidi na mustakabali wenye
usawa zaidi
“Mijadala katika maeneo hayo ya kipaumbele itahusisha masuala
mbalimbali ikiwemo kukuza zaidi biashara na uwekezaji baina ya nchi
za Jumuiya ya Madola kwa manufaa ya nchi wanachama na Jumuiya
nzima
Pia, kukuza na kuendeleza misingi ya demokrasia, ajenda ya
mabadiliko ya tabia nchi na maendeleo endelevu pamoja pamoja na
masuala ya uhalifu wa kimataifa kama vile ugaidi, uhalifu wa
kimtandao na usafirishaji wa binadamu
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Makamu wa Rais amembana na Waziri
wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Dk Augustine Mahiga pamoja na viongozi wengine
waandamizi kutoka wizara hiyo ambapo msafara huo unatarajia
kurejea nchini Aprili 22.
Makamu wa Rais kumwakilisha JPM Uingereza
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment