Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima
ameeleza namna alivyonyang’anywa samani na muumini wake siku chache baada ya
kumkabidhi
Akitoa mahubiri katika ibada leo Aprili 15,2018 kanisani
kwake, Ubungo jijini Dar es Salaam, Askofu Gwajima amesema aliamua
kumrudishia muumini huyo na kukubali kuaibika
Akisimulia kisa hicho mbele ya mamia ya waumini, Askofu
Gwajima amesema wakati anaanza maisha na kazi ya kuendesha kanisa hilo,
alipanga chumba kimoja katika eneo la Ubungo Msewe
“Katika chumba nilichokuwa nimepanga kitu cha thamani
nilichokuwa nacho ilikuwa ni carpet (zuria) la plastiki,” amesema
Amesema wakati akiendelea kuishi katika chumba hicho,
alitembelewa na muumini wake aliyemtaja kwa jina moja la Ester
“Ester baada ya kuona mazingira ya chumba kile, akaniambia
mchungaji hapa panahitajika stuli kwa ajili ya kukalia, nitazileta,” amesema
Askofu Gwajima ameisema kweli muumini huyo alimpelekea stuli
nne na yeye akamshukuru kwa msaada huo
“Baadaye muumini huyo akawa anatamba kanisani akiwaeleza
waumini wenzake kwamba stuli zilizoko kwa mchungaji zimepelekwa na yeye,”
amesema
Gwajima amesema muumini huyo akawa anataka waumini wenzake
wathamini mchango ambao anautoa kwa mchungaji
“Baada ya kusikia hilo kutoka tulimwita na kumuonya
asiwatishe waumini kwa kutumia kigezo cha msaada huo,” amesema
Ameongeza, “siku moja nilitembelewa na ndugu zangu akiwemo
mjomba, wakakaa kwenye stuli zile. baada ya muda mfupi Ester akaingia na kudai
stuli zake mbele ya ndugu zangu.”
“Nikamtoa nje ili tuzungumze lakini msimamo wake ukawa
uleule apewe stuli zake, ndugu zangu wakawa wanashangaa hawaamini
kinachotokea,” amesema
“Mjomba wangu akanieleza kwamba ina maana Gwajima huna hata
stuli kwenye chumba chako
“Nikamwambia stuli hizo si mali yangu ni za muumini hivyo
nikawataka wageni wale wakae kwenye zuria, nikampa stuli zake.”
Amewataka waumini hao wasiogope kuaibishwa na mtu kwa sababu
hatima ya maisha yao ipo palepale
“Ni kweli niliaibishwa mbele ya ndugu zangu lakini sikukata
tamaa na hatima ya maisha yangu ilikuwa palepale kama mnavyoniona leo,”
amesema.
ASKOFU GWAJIMA MUUMINI WANGU ALINIABISHA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment