Kesi ya mauaji ya kukusudia ya mfanyabiashara tajiri wa
madini, Erasto Msuya ambayo iliahirishwa Februari mwaka huu kwa
kukosekana mashahidi, imepangwa kuendelea kusikilizwa kesho Aprili 16
Kuanzia Februari 20 hadi 23, upande wa mashtaka ulikuwa
ukiomba kesi iahirishwe kwa kuwa walikuwa hawana shahidi licha ya kuiambia
mahakama kuwa wana jumla ya mashahidi
Wakati jopo la mawakili wa Serikali linaloongozwa na Wakili
wa Serikali Mkuu, Peter Maugo likijikuta katika sintofahamu hiyo, upande wa
mashtaka ulikuwa umefanikiwa kuita mashahidi 25 kati ya 50
Februari 21, 22 na 23, Wakili Maugo anayesaidiana na
mawakili waandamizi Abdalah Chavula, Omary Kibwana na Kassim Nassir alijikuta
katika kibarua kigumu cha kuiomba mahakama kwa siku tatu mfululizo iahirishe
kesi hiyo kwa tatizo hilo
Wakili Majura Magafu ambaye ni miongoni mwa mawakili wanne
wanaowatetea washtakiwa alikaririwa kipindi hicho akisema wamesikia shida
wanayopata upande wa mashtaka katika kuleta mashahidi, lakini akaomba
wajitahidi ili wapatikane
“Tumesikia concern (ombi) yao lakini tunaomba wajitahidi
kuhakikisha wanapatikana kwa sababu record (kumbukumbu) zao na anuani zao zipo
na wanafahamika,” alisema Magafu
Mauaji ya mfanyabiashara huyo yalifanyika Agosti 7, 2013
Kesi hiyo inayovuta hisia za wengi inawakabili washtakiwa
saba ambao ni Sharifu Mohamed, Shaibu Jumanne, Mussa Mangu, Jalila Zuberi,
Karim Kihundwa, Sadick Jabir na Ally Mussa
Kesi ya Bilionea Msuya kuendelea kesho
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment