Majambazi wamevamia Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu-Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam na kupora fedha na baadhi ya vifaa vya kuendeshea misa usiku wa kuamkia leo
Akizungumza na Mwananchi, Mwenyekiti wa
Kamati ya Mipango, Uchumi na Fedha wa parokia hiyo, Arnold Kimanganu amesema
kuwa majambazi hao waliwapiga walinzi kabla ya kuingia kanisani
“Majambazi walivyofika waliwapiga walinzi,
tuna walinzi wanne walimshika mlinzi mwenye silaha wakampiga na kumnyang’anya
bunduki, kumkamata mwingine wakampiga na kumfunga na wakaingia sehemu inaitwa
sakristia, wakavunja milango ya sakristia wakakusanya matoleo yote yaliyokuwa
yamehifadhiwa yaliyokusanywa kipindi cha pasaka,” amesema Kimanganu
Paroko wa parokia hiyo, Sunil Kishor amesema
majambazi hao walivamia kanisa hilo saa tisa usiku na wameiba fedha na baadhi
ya vifaa vya kuendesha misa
“Ni kweli majambazi walivamia kanisa letu
majira ya saa tisa alfajiri, walichochukua kuna pesa za sadaka ambazo
zilikuwepo sakristia, vifaa vya misa hasa vikombe na siborio,” amesema Paroko
Kishor na kuongeza kuwa
“Kiasi cha fedha ambacho wamechukua kadri ya
hesabu ni kama milioni nane hivi, Tumesharipoti polisi na wapo hapa kanisani
wanaendelea na uchunguzi.”
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekiri kutokea ingawa bado
hajapata taarifa ofisini kwake kimaandishi
‘’Ni kweli vibaka walivamia na wameiba
sadaka, lakini bado sijalipata vizuri tukio hili nikilipata nitalitolea
taarifa, lakini nathibitisha kutokea kwa tukio hilo,” amesema Kamanda Mambosasa.
Majambazi wavamia na kuvunja kanisa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 05, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment